1 Wafalme 11:39
1 Kings 11:39 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nitawatesa wazao wa Daudi kwa ajili ya hili, lakini siyo milele.’ ”
1 Kings 11:39 in English
1 Kings 11:39 · Berean Standard Bible
Because of this, I will humble David’s descendants—but not forever.’”
Context
37Hata hivyo, kukuhusu wewe Yeroboamu, nitakutwaa, nawe utatawala juu ya yote yale moyo wako unayotamani, utakuwa mfalme juu ya Israeli. 38Ikiwa utafanya kila nitakalokuamuru, kuenenda katika njia zangu na kufanya yaliyo sawa mbele za macho yangu kwa kuzishika amri zangu na maagizo yangu kama alivyofanya Daudi mtumishi wangu, nitakuwa pamoja nawe. Nitakujengea ufalme utakaodumu kama ule niliomjengea Daudi, nami nitakupa Israeli. 39Nitawatesa wazao wa Daudi kwa ajili ya hili, lakini siyo milele.’ ” 40Solomoni akajaribu kumuua Yeroboamu, lakini Yeroboamu akakimbilia Misri, kwa Mfalme Shishaki, naye akakaa huko mpaka Solomoni alipofariki. 41Kwa habari za matukio mengine ya utawala wa Solomoni, yote aliyoyafanya na hekima aliyoionyesha, je hayakuandikwa yote katika kitabu cha matendo cha Solomoni?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.