Native Bible

1 Kings 11:37 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hata hivyo, kukuhusu wewe Yeroboamu, nitakutwaa, nawe utatawala juu ya yote yale moyo wako unayotamani, utakuwa mfalme juu ya Israeli.

1 Kings 11:37 in English

1 Kings 11:37 · Berean Standard Bible

But as for you, I will take you, and you shall reign over all that your heart desires, and you will be king over Israel.

Context

35Nitauondoa ufalme kutoka mikononi mwa mwanawe na kukupa wewe makabila kumi. 36Nitampa mwanawe kabila moja ili kwamba Daudi mtumishi wangu awe na taa mbele zangu daima katika Yerusalemu, mji ambao nimeuchagua kuweka Jina langu. 37Hata hivyo, kukuhusu wewe Yeroboamu, nitakutwaa, nawe utatawala juu ya yote yale moyo wako unayotamani, utakuwa mfalme juu ya Israeli. 38Ikiwa utafanya kila nitakalokuamuru, kuenenda katika njia zangu na kufanya yaliyo sawa mbele za macho yangu kwa kuzishika amri zangu na maagizo yangu kama alivyofanya Daudi mtumishi wangu, nitakuwa pamoja nawe. Nitakujengea ufalme utakaodumu kama ule niliomjengea Daudi, nami nitakupa Israeli. 39Nitawatesa wazao wa Daudi kwa ajili ya hili, lakini siyo milele.’ ”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.