Native Bible

1 John 5:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Jambo lolote lisilo la haki ni dhambi, lakini iko dhambi isiyo ya mauti.

1 John 5:17 in English

1 John 5:17 · Berean Standard Bible

All unrighteousness is sin, yet there is sin that does not lead to death.

Context

15Nasi kama tunajua atusikia, lolote tuombalo, tunajua ya kwamba tumekwisha kupata zile haja tulizomwomba. 16Kama mtu akimwona ndugu yake akitenda dhambi isiyo ya mauti, inampasa aombe, naye Mungu atampa uzima mtu huyo. Ninamaanisha wale ambao dhambi yao si ya mauti. Iko dhambi ya mauti, sisemi kwamba utaomba kwa ajili ya hiyo. 17Jambo lolote lisilo la haki ni dhambi, lakini iko dhambi isiyo ya mauti. 18Tunajua ya kuwa yeye aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, bali aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hawezi kumdhuru. 19Sisi twajua kuwa tu watoto wa Mungu na ya kwamba ulimwengu wote uko chini ya utawala wa yule mwovu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.