1 Yohana 2:26
1 John 2:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nawaandikia mambo haya kuhusu wale watu ambao wanajaribu kuwapotosha.
1 John 2:26 in English
1 John 2:26 · Berean Standard Bible
I have written these things to you about those who are trying to deceive you.
Context
24Hakikisheni kwamba lile mlilosikia tangu mwanzo linakaa ndani yenu. Kama lile mlilosikia tangu mwanzo linakaa ndani yenu, ninyi nanyi mtakaa ndani ya Mwana na ndani ya Baba. 25Hii ndiyo ahadi yake kwetu, yaani, uzima wa milele. 26Nawaandikia mambo haya kuhusu wale watu ambao wanajaribu kuwapotosha. 27Nanyi, upako mlioupata kutoka kwake unakaa ndani yenu, wala ninyi hamna haja ya mtu yeyote kuwafundisha. Lakini kama vile upako wake unavyowafundisha kuhusu mambo yote nayo ni kweli wala si uongo, basi kama ulivyowafundisha kaeni ndani yake. 28Sasa basi, watoto wapendwa, kaeni ndani yake, ili atakapofunuliwa, tuwe na ujasiri, wala tusiaibike mbele zake wakati wa kuja kwake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.