Native Bible

1 Corinthians 4:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Lakini kama Bwana akipenda, nitafika kwenu mapema, nami nitapenda kujua, si tu kile wanachosema hawa watu jeuri, bali pia kujua nguvu yao.

1 Corinthians 4:19 in English

1 Corinthians 4:19 · Berean Standard Bible

But I will come to you shortly, if the Lord is willing, and then I will find out not only what these arrogant people are saying, but what power they have.

Context

17Kwa sababu hii ninamtuma Timotheo, mwanangu mpendwa na mwaminifu katika Bwana. Yeye atawakumbusha kuhusu njia za maisha yangu katika Kristo Yesu, ambayo yanakubaliana na mafundisho yangu ninayofundisha katika kila kanisa. 18Baadhi yenu mmekuwa na jeuri mkidhani kuwa sitafika kwenu. 19Lakini kama Bwana akipenda, nitafika kwenu mapema, nami nitapenda kujua, si tu kile wanachosema hawa watu jeuri, bali pia kujua nguvu yao. 20Kwa kuwa Ufalme wa Mungu si maneno matupu tu bali ni nguvu. 21Ninyi amueni. Je, nije kwenu na fimbo, au nije kwa upendo na kwa roho ya upole?

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.