Native Bible

1 Corinthians 15:46 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Lakini si ule wa kiroho uliotangulia, bali ni ule wa asili, kisha ule wa kiroho.

1 Corinthians 15:46 in English

1 Corinthians 15:46 · Berean Standard Bible

The spiritual, however, was not first, but the natural, and then the spiritual.

Context

44unapandwa mwili wa asili, unafufuliwa mwili wa kiroho. Kama kuna mwili wa asili, basi kuna mwili wa kiroho pia. 45Kwa hiyo imeandikwa, “Mtu wa kwanza Adamu alifanyika kiumbe hai”; Adamu wa mwisho, yeye ni roho iletayo uzima. 46Lakini si ule wa kiroho uliotangulia, bali ni ule wa asili, kisha ule wa kiroho. 47Mtu wa kwanza aliumbwa kwa mavumbi ya ardhini, mtu wa pili alitoka mbinguni. 48Kama vile alivyokuwa yule wa ardhini, ndivyo walivyo wale walio wa ardhini; na kwa vile alivyo mtu yule aliyetoka mbinguni, ndivyo walivyo wale walio wa mbinguni.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.