1 Wakorintho 14:29
1 Corinthians 14:29 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Manabii wawili au watatu wanene na wengine wapime yale yasemwayo.
1 Corinthians 14:29 in English
1 Corinthians 14:29 · Berean Standard Bible
Two or three prophets should speak, and the others should weigh carefully what is said.
Context
27Kama mtu yeyote akinena kwa lugha, basi waseme watu wawili au watatu si zaidi, mmoja baada ya mwingine na lazima awepo mtu wa kutafsiri. 28Lakini kama hakuna mtu wa kutafsiri, hao watu na wanyamaze kimya kanisani na wanene na nafsi zao wenyewe na Mungu. 29Manabii wawili au watatu wanene na wengine wapime yale yasemwayo. 30Kama mtu yeyote aliyeketi karibu, akipata ufunuo, basi yule wa kwanza na anyamaze. 31Kwa maana wote mnaweza kutoa unabii, mmoja baada ya mwingine, ili kila mtu apate kufundishwa na kutiwa moyo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.