1 Wakorintho 13:9
1 Corinthians 13:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa maana tunafahamu kwa sehemu na tunatoa unabii kwa sehemu.
1 Corinthians 13:9 in English
1 Corinthians 13:9 · Berean Standard Bible
For we know in part and we prophesy in part,
Context
7Upendo huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote. 8Upendo haushindwi kamwe. Lakini ukiwepo unabii, utakoma; zikiwepo lugha, zitakoma; yakiwepo maarifa, yatapita. 9Kwa maana tunafahamu kwa sehemu na tunatoa unabii kwa sehemu. 10Lakini ukamilifu ukija, yale yasiyo kamili hutoweka. 11Nilipokuwa mtoto, nilisema kama mtoto, niliwaza kama mtoto, nilifikiri kama mtoto. Nilipokuwa mtu mzima niliacha mambo ya kitoto.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.