1 Wakorintho 13:4
1 Corinthians 13:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Upendo huvumilia, upendo hufadhili, upendo hauoni wivu, hauna majivuno, hauna kiburi.
1 Corinthians 13:4 in English
1 Corinthians 13:4 · Berean Standard Bible
Love is patient, love is kind. It does not envy, it does not boast, it is not proud.
Context
2Ningekuwa na karama ya unabii na kujua siri zote na maarifa yote, hata kama nina imani kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, mimi si kitu. 3Kama nikitoa mali yote niliyo nayo na kama nikijitolea mwili wangu uchomwe moto, kama sina upendo, hainifaidi kitu. 4Upendo huvumilia, upendo hufadhili, upendo hauoni wivu, hauna majivuno, hauna kiburi. 5Haukosi kuwa na adabu, hautafuti mambo yake, haukasiriki upesi, hauweki kumbukumbu ya mabaya. 6Upendo haufurahii mabaya bali hufurahi pamoja na kweli.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.