1 Wakorintho 1:8
1 Corinthians 1:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Atawafanya imara mpaka mwisho, ili msiwe na hatia siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo.
1 Corinthians 1:8 in English
1 Corinthians 1:8 · Berean Standard Bible
He will sustain you to the end, so that you will be blameless on the day of our Lord Jesus Christ.
Context
6kwa sababu ushuhuda wetu kumhusu Kristo ulithibitishwa ndani yenu. 7Kwa hiyo hamkupungukiwa na karama yoyote ya kiroho wakati mnangoja kwa shauku kudhihirishwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo. 8Atawafanya imara mpaka mwisho, ili msiwe na hatia siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo. 9Mungu ambaye mmeitwa naye ili mwe na ushirika na Mwanawe Yesu Kristo, Bwana wetu ni mwaminifu. 10Nawasihi ndugu zangu, katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi, ili pasiwepo na matengano katikati yenu na kwamba mwe na umoja kikamilifu katika nia na katika kusudi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.