1 Nyakati 9:30
1 Chronicles 9:30 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini baadhi ya makuhani walifanya kazi ya kuchanganya vikolezo.
1 Chronicles 9:30 in English
1 Chronicles 9:30 · Berean Standard Bible
And some of the sons of the priests mixed the spices.
Context
28Baadhi yao walikuwa viongozi wa kutunza vifaa vilivyotumika katika huduma ndani ya Hekalu; walivihesabu kila vilipoingizwa ndani na kila vilipotolewa. 29Wengine walipangiwa kutunza mapambo na vifaa vingine vya patakatifu, pamoja na unga, divai, mafuta, uvumba na vikolezo. 30Lakini baadhi ya makuhani walifanya kazi ya kuchanganya vikolezo. 31Mlawi aliyeitwa Matithia, mwana mzaliwa wa kwanza wa Shalumu, wa ukoo wa Kora, alikabidhiwa wajibu kwa ajili ya kuoka mikate ya sadaka. 32Baadhi ya ndugu zao wa ukoo wa Kohathi walikuwa viongozi wa kuandaa mikate ya Wonyesho kwa ajili ya kila Sabato, mikate iliyokuwa inawekwa mezani.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.