1 Nyakati 9:28
1 Chronicles 9:28 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Baadhi yao walikuwa viongozi wa kutunza vifaa vilivyotumika katika huduma ndani ya Hekalu; walivihesabu kila vilipoingizwa ndani na kila vilipotolewa.
1 Chronicles 9:28 in English
1 Chronicles 9:28 · Berean Standard Bible
Some of them were in charge of the articles used in worship, to count them whenever they were brought in or taken out.
Context
26Lakini mabawabu wanne wakuu, waliokuwa Walawi, walikabidhiwa wajibu kwa ajili ya vyumba na hazina katika nyumba ya Mungu. 27Walikesha mahali walipowekwa kuizunguka nyumba ya Mungu, kwa sababu iliwapasa kuilinda. Pia walitunza funguo kwa ajili ya kufungua mlango kila siku asubuhi. 28Baadhi yao walikuwa viongozi wa kutunza vifaa vilivyotumika katika huduma ndani ya Hekalu; walivihesabu kila vilipoingizwa ndani na kila vilipotolewa. 29Wengine walipangiwa kutunza mapambo na vifaa vingine vya patakatifu, pamoja na unga, divai, mafuta, uvumba na vikolezo. 30Lakini baadhi ya makuhani walifanya kazi ya kuchanganya vikolezo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.