1 Nyakati 9:24
1 Chronicles 9:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mabawabu walikuwa pande zote nne: mashariki, magharibi, kaskazini na kusini.
1 Chronicles 9:24 in English
1 Chronicles 9:24 · Berean Standard Bible
The gatekeepers were stationed on the four sides: east, west, north, and south.
Context
22Jumla ya waliochaguliwa kuwa mabawabu katika sakafu za kupuria nafaka walikuwa watu 212. Waliandikishwa kwa koo zao kwenye vijiji vyao. Mabawabu hawa waliwekwa katika nafasi zao za kuaminiwa na Daudi pamoja na mwonaji Samweli. 23Wao na wazao wao walikuwa viongozi wa kulinda malango ya nyumba ya Bwana, nyumba iliyoitwa Hema. 24Mabawabu walikuwa pande zote nne: mashariki, magharibi, kaskazini na kusini. 25Ndugu zao katika vijiji vyao walikuwa wakija mara kwa mara na kuwasaidia katika kazi zao kwa vipindi mbalimbali vya siku saba. 26Lakini mabawabu wanne wakuu, waliokuwa Walawi, walikabidhiwa wajibu kwa ajili ya vyumba na hazina katika nyumba ya Mungu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.