1 Nyakati 9:18
1 Chronicles 9:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Walikuwa wamewekwa katika lango la mfalme lililokuwa upande wa mashariki, mpaka wakati huu. Hawa walikuwa mabawabu wa kutoka kwenye kambi ya Walawi.
1 Chronicles 9:18 in English
1 Chronicles 9:18 · Berean Standard Bible
he was previously stationed at the King’s Gate on the east side. These were the gatekeepers from the camp of the Levites.
Context
16Obadia mwana wa Shemaya, mwana wa Galali, mwana wa Yeduthuni. Berekia mwana wa Asa, mwana wa Elikana, ambao waliishi katika vijiji vya Wanetofathi. 17Mabawabu katika Hekalu la Bwana waliorudi walikuwa:
Shalumu, Akubu, Talmoni, Ahimani na ndugu zao. Shalumu alikuwa mlinzi wao mkuu. 18Walikuwa wamewekwa katika lango la mfalme lililokuwa upande wa mashariki, mpaka wakati huu. Hawa walikuwa mabawabu wa kutoka kwenye kambi ya Walawi. 19Shalumu mwana wa Kore, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora, pamoja na mabawabu wenzake kutoka jamaa yake ya Kora waliwajibika kulinda malango ya Hema, kama vile baba zao walivyokuwa wamewajibika kulinda ingilio la Maskani ya Bwana. 20Hapo zamani Finehasi mwana wa Eleazari alikuwa kiongozi wa mabawabu, naye Bwana alikuwa pamoja naye:
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.