1 Nyakati 23:26
1 Chronicles 23:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Walawi hawahitaji tena kubeba Maskani wala chombo chochote cha utumishi wake.”
1 Chronicles 23:26 in English
1 Chronicles 23:26 · Berean Standard Bible
So now the Levites no longer need to carry the tabernacle or any of the articles for its service.”
Context
24Hawa walikuwa wazao wa Lawi kwa jamaa zao. Wakuu wa jamaa kama walivyoandikwa kwa majina yao na kuhesabiwa kila mmoja, yaani, wenye uwezo wa kufanya kazi kuanzia miaka ishirini au zaidi, waliohudumu katika Hekalu la Bwana. 25Kwa maana Daudi alikuwa amesema, “Kwa vile Bwana, Mungu wa Israeli amewapa watu wake raha na amekuja kuishi Yerusalemu milele, 26Walawi hawahitaji tena kubeba Maskani wala chombo chochote cha utumishi wake.” 27Kulingana na maagizo ya mwisho ya Daudi, Walawi waliohesabiwa ni wale wa kuanzia umri wa miaka ishirini au zaidi. 28Wajibu wa Walawi ulikuwa kuwasaidia wazao wa Aroni kuhudumu katika Hekalu la Bwana: Kuwa wasimamizi wa nyua, vyumba vya pembeni, kutakasa vyombo vitakatifu na utendaji mwingine wowote katika nyumba ya Mungu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.