Native Bible

1 Chronicles 21:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Shetani akainuka dhidi ya Israeli na kumshawishi Daudi ahesabu watu wa Israeli.

1 Chronicles 21:1 in English

1 Chronicles 21:1 · Berean Standard Bible

Then Satan * rose up against Israel and incited David to take a census of Israel.

Context

1Shetani akainuka dhidi ya Israeli na kumshawishi Daudi ahesabu watu wa Israeli. 2Kwa hiyo Daudi akamwambia Yoabu na majemadari wa jeshi, “Nendeni mkawahesabu Waisraeli kuanzia Beer-Sheba mpaka Dani. Kisha nileteeni taarifa ili kwamba niweze kufahamu wako wangapi.” 3Yoabu akajibu, “Bwana na aongeze jeshi lake mara mia na zaidi. Mfalme bwana wangu, kwani hawa wote si raiya wa bwana wangu? Kwa nini bwana wangu unataka kufanya hivi? Kwa nini kuleta hatia juu ya Israeli?”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.