1 Nyakati 20:7
1 Chronicles 20:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Alipowadhihaki Israeli, Yonathani, mwana wa Shimea, nduguye Daudi, akamuua.
1 Chronicles 20:7 in English
1 Chronicles 20:7 · Berean Standard Bible
and when he taunted Israel, Jonathan the son of David’s brother Shimei killed him.
Context
5Katika vita vingine na Wafilisti, Elhanani mwana wa Yairi alimuua Lahmi nduguye Goliathi, Mgiti, ambaye mkuki wake ulikuwa na mpini kama mti wa mfumaji. 6Katika vita vingine tena, vilivyopiganwa huko Gathi, kulikuwako na mtu mmoja mkubwa mwenye vidole sita katika kila mkono na vidole sita katika kila mguu: jumla vidole ishirini na vinne. Yeye alikuwa pia mzao wa Mrefai. 7Alipowadhihaki Israeli, Yonathani, mwana wa Shimea, nduguye Daudi, akamuua. 8Hawa walikuwa ndio wazao wa Warefai huko Gathi, nao walianguka kwa mikono ya Daudi na watu wake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.