Native Bible

1 Chronicles 15:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Berekia na Elikana walikuwa mabawabu kwa ajili ya Sanduku.

1 Chronicles 15:23 in English

1 Chronicles 15:23 · Berean Standard Bible

Berechiah and Elkanah were to be guardians * of the ark.

Context

21na Matithia, Elifelehu, Mikneya, Obed-Edomu, Yehieli na Azazia walikuwa wapiga vinubi, wakiongozwa kwa kufuata sauti ya sheminithi .* 22Kenania kiongozi wa Walawi alikuwa msimamizi wa uimbaji; huu ndio uliokuwa wajibu wake kwa sababu alikuwa stadi katika hilo. 23Berekia na Elikana walikuwa mabawabu kwa ajili ya Sanduku. 24Shebania, Yoshafati, Nethaneli, Amasai, Zekaria, Benaya na Eliezeri, makuhani, walikuwa wapiga tarumbeta mbele ya Sanduku la Mungu. Obed-Edomu na Yehiya waliwekwa pia kuwa mabawabu wa Sanduku. 25Basi Daudi pamoja na wazee wa Israeli na majemadari wa vikosi vya elfu wakaenda ili kulipandisha Sanduku la Agano la Bwana kutoka nyumba ya Obed-Edomu kwa shangwe.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.