1 Nyakati 10:8
1 Chronicles 10:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kesho yake Wafilisti walipokuja kuwavua maiti silaha, walimkuta Sauli na wanawe wameanguka katika Mlima Gilboa.
1 Chronicles 10:8 in English
1 Chronicles 10:8 · Berean Standard Bible
The next day, when the Philistines came to strip the dead, they found Saul and his sons fallen on Mount Gilboa.
Context
6Kwa hiyo Sauli na wanawe watatu wakafa, pamoja na nyumba yake yote. 7Waisraeli wote waliokuwa bondeni walipoona kwamba jeshi limekimbia na kwamba Sauli na wanawe wamekufa, waliacha miji yao wakakimbia. Nao Wafilisti wakaja na kukaa humo. 8Kesho yake Wafilisti walipokuja kuwavua maiti silaha, walimkuta Sauli na wanawe wameanguka katika Mlima Gilboa. 9Wakamvua mavazi, wakachukua kichwa chake pamoja na silaha zake, wakawatuma wajumbe katika nchi yote ya Wafilisti kutangaza habari hizi miongoni mwa sanamu zao na watu wao. 10Waliweka silaha zake katika hekalu la miungu yao, wakatundika kichwa chake katika hekalu la Dagoni.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.