Native Bible

Zechariah 7:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote: ‘Fanyeni hukumu za haki, onyesheni rehema na huruma ninyi kwa ninyi.

Zechariah 7:9 in English

Zechariah 7:9 · Berean Standard Bible

“This is what the LORD of Hosts says: ‘Administer true justice. Show loving devotion * and compassion to one another.

Context

7Je, haya sio maneno ya Bwana aliyosema kupitia manabii waliotangulia, wakati Yerusalemu pamoja na miji inayoizunguka ilipokuwa katika hali ya utulivu na ya mafanikio, wakati Negebu na Shefala zikiwa zimekaliwa na watu?’ ” 8Neno la Bwana likamjia tena Zekaria: 9“Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote: ‘Fanyeni hukumu za haki, onyesheni rehema na huruma ninyi kwa ninyi. 10Msimwonee mjane wala yatima, mgeni wala maskini. Msiwaziane mabaya mioyoni mwenu ninyi kwa ninyi.’ 11“Lakini wakakataa kusikiliza, wakanipa kisogo kwa ukaidi na kuziba masikio yao.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.