Zekaria 7:2
Zechariah 7:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Watu wa Betheli walikuwa wamemtuma Shareza na Regem-Meleki pamoja na watu wao, kumsihi Bwana
Zechariah 7:2 in English
Zechariah 7:2 · Berean Standard Bible
Now the people of Bethel had sent Sharezer and Regem-melech, along with their men,* to plead before the LORD
Context
1Katika mwaka wa nne wa utawala wa Mfalme Dario, neno la Bwana lilimjia Zekaria siku ya nne ya mwezi wa tisa, mwezi wa Kisleu. 2Watu wa Betheli walikuwa wamemtuma Shareza na Regem-Meleki pamoja na watu wao, kumsihi Bwana 3kwa kuwauliza makuhani wa nyumba ya Bwana Mwenye Nguvu Zote na manabii, “Je, imempasa kuomboleza na kufunga katika mwezi wa tano, kama ambavyo nimekuwa nikifanya kwa miaka mingi?” 4Kisha neno la Bwana Mwenye Nguvu Zote likanijia kusema:
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.