Ruthu 3:5
Ruth 3:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ruthu akajibu, “Lolote usemalo nitatenda.”
Ruth 3:5 in English
Ruth 3:5 · Berean Standard Bible
“I will do everything you say,” Ruth answered.
Context
3Basi oga na ukajipake marashi, ujivalie nguo zako nzuri. Kisha uende kwenye sakafu ya kupuria, lakini angalia asijue kwamba upo pale mpaka atakapomaliza kula na kunywa. 4Atakapokwenda kulala, angalia mahali atakapolala. Kisha uende ufunue miguu yake, ulale. Naye atakuambia utakalofanya.” 5Ruthu akajibu, “Lolote usemalo nitatenda.” 6Basi akashuka mpaka kwenye sakafu ya kupuria, akafanya kila kitu mama mkwe wake alichomwambia kufanya. 7Wakati Boazi alipomaliza kula na kunywa, naye akawa amejawa na furaha, alikwenda kulala mwisho wa lundo la nafaka. Ruthu akanyemelea polepole, akafunua miguu yake, na akalala.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.