Native Bible

Ruth 2:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Badala yake, toeni masuke katika miganda, mwachieni ayaokote, na msimkemee.”

Ruth 2:16 in English

Ruth 2:16 · Berean Standard Bible

Rather, pull out for her some stalks from the bundles and leave them for her to gather. Do not rebuke her.”

Context

14Wakati wa chakula, Boazi akamwambia Ruthu, “Karibia hapa. Kula mkate na uchovye ndani ya siki.” Alipoketi pamoja na wavunaji, akampa nafaka zilizookwa. Akala kiasi alichotaka na kusaza. 15Alipoinuka ili kuokota mabaki ya nafaka, Boazi akawaagiza watu wake, “Hata kama atakusanya kati ya miganda, msimzuie. 16Badala yake, toeni masuke katika miganda, mwachieni ayaokote, na msimkemee.” 17Basi Ruthu akaokota masazo shambani hata jioni. Akatwanga ile shayiri aliyokusanya, ikajaa efa moja.* 18Akaibeba na kuelekea mjini, naye mama mkwe wake akaona jinsi alivyoweza kuokota nafaka nyingi. Pia Ruthu akachukua kile alichobakiza baada ya kula na kushiba, akampa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.