Ruthu 1:18
Ruth 1:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Naomi alipotambua kwamba Ruthu amenuia kufuatana naye, hakuendelea kumsihi tena.
Ruth 1:18 in English
Ruth 1:18 · Berean Standard Bible
When Naomi saw that Ruth was determined to go with her, she stopped trying to persuade her.
Context
16Lakini Ruthu akajibu, “Usinisihi nikuache au niache kukufuata. Utakakokwenda nami nitakwenda, na wewe utakapoishi nitaishi. Watu wako watakuwa watu wangu, na Mungu wako atakuwa Mungu wangu. 17Pale utakapofia nami nitafia hapo, na papo hapo nitazikwa. Bwana na aniadhibu vikali, kama kitu kingine chochote kitanitenga nawe isipokuwa kifo.” 18Naomi alipotambua kwamba Ruthu amenuia kufuatana naye, hakuendelea kumsihi tena. 19Kwa hiyo hao wanawake wawili wakaondoka, wakafika Bethlehemu. Walipofika Bethlehemu, mji mzima ulitaharuki, wanawake wakashangaa, wakasema, “Huyu aweza kuwa ni Naomi?” 20Akawaambia, “Msiniite tena Naomi,* niiteni Mara,* kwa sababu Mwenyezi* amenitendea mambo machungu sana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.