Warumi 2:19
Romans 2:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
kama unatambua kuwa wewe ni kiongozi wa vipofu, na mwanga kwa wale walio gizani,
Romans 2:19 in English
Romans 2:19 · Berean Standard Bible
if you are convinced that you are a guide for the blind, a light for those in darkness,
Context
17Tazama, wewe ukiwa unaitwa Myahudi na kuitegemea sheria na kujisifia uhusiano wako na Mungu, 18kama unajua mapenzi ya Mungu na kukubali lililo bora kwa sababu umefundishwa na hiyo sheria, 19kama unatambua kuwa wewe ni kiongozi wa vipofu, na mwanga kwa wale walio gizani, 20mkufunzi wa wajinga na mwalimu wa watoto wachanga, kwa kuwa una maarifa ya kweli katika hiyo sheria, 21basi wewe, uwafundishaye wengine, mbona hujifunzi mwenyewe? Wewe uhubiriye kwamba mtu asiibe, wewe mwenyewe waiba?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.