Warumi 10:6
Romans 10:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini ile haki itokanayo na imani husema hivi: “Usiseme moyoni mwako, ‘Ni nani atakayepanda mbinguni?’ ” (yaani ili kumleta Kristo chini)
Romans 10:6 in English
Romans 10:6 · Berean Standard Bible
But the righteousness that is by faith says: “Do not say in your heart, ‘Who will ascend into heaven?’* (that is, to bring Christ down)
Context
4Kwa maana Kristo ni ukomo wa sheria ili kuwe na haki kwa kila mtu aaminiye. 5Mose anaandika kuhusu haki ile itokanayo na sheria, kwamba, “Mtu atendaye matendo hayo ataishi kwa hayo.” 6Lakini ile haki itokanayo na imani husema hivi: “Usiseme moyoni mwako, ‘Ni nani atakayepanda mbinguni?’ ” (yaani ili kumleta Kristo chini) 7“au ‘Ni nani atashuka kwenda kuzimu?’ ” (yaani ili kumleta Kristo kutoka kwa wafu.) 8Lakini andiko lasemaje? “Lile neno liko karibu nawe, liko kinywani mwako na moyoni mwako,” yaani, lile neno la imani tunalolihubiri.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.