Ufunuo 3:6
Revelation 3:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho ayaambia makanisa.
Revelation 3:6 in English
Revelation 3:6 · Berean Standard Bible
He who has an ear, let him hear what the Spirit says to the churches.
Context
4“Lakini bado una watu wachache katika Sardi ambao hawajayachafua mavazi yao. Wao wataenda pamoja nami, wakiwa wamevaa mavazi meupe, kwa maana wanastahili. 5Yeye ashindaye atavikwa vazi jeupe kama wao. Sitafuta jina lake kutoka kitabu cha uzima, bali nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu na mbele za malaika wake. 6Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho ayaambia makanisa. 7“Kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika:
“Haya ndiyo maneno yake yeye aliye mtakatifu na wa kweli, yeye aliye na ufunguo wa Daudi. Anachokifungua hakuna awezaye kukifunga, wala anachokifunga hakuna awezaye kukifungua. 8Nayajua matendo yako. Tazama, nimeweka mbele yako mlango uliofunguliwa, wala hakuna awezaye kuufunga. Ninajua kwamba una nguvu kidogo lakini umelishika neno langu wala hukulikana Jina langu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.