Ufunuo 3:1
Revelation 3:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika: “Haya ndiyo maneno ya aliye na zile Roho saba* za Mungu na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, kwamba una sifa ya kuwa hai, lakini umekufa.
Revelation 3:1 in English
Revelation 3:1 · Berean Standard Bible
“To the angel of the church in Sardis write: These are the words of the One who holds the seven Spirits * of God and the seven stars. I know your deeds; you have a reputation for being alive, yet you are dead.
Context
1“Kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika:
“Haya ndiyo maneno ya aliye na zile Roho saba* za Mungu na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, kwamba una sifa ya kuwa hai, lakini umekufa. 2Amka! Nawe uyaimarishe yale yaliyosalia na yaliyo karibu kufa, kwa maana sikuona kwamba kazi zako zimekamilika machoni pa Mungu wangu. 3Kumbuka basi yale uliyoyapokea na kuyasikia, yatii na ukatubu. Lakini usipoamka, nitakuja kama mwizi wala hutajua saa nitakayokuja kwako.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.