Ufunuo 19:14
Revelation 19:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Majeshi ya mbinguni walikuwa wakimfuata, wakiwa wamepanda farasi weupe, hali wamevaa mavazi ya kitani safi, nyeupe na nzuri.
Revelation 19:14 in English
Revelation 19:14 · Berean Standard Bible
The armies of heaven, dressed in fine linen, white and pure, follow Him on white horses.
Context
12Macho yake ni kama miali ya moto na juu ya kichwa chake kuna taji nyingi. Ana jina lililoandikwa ambalo hakuna mtu yeyote anayelijua isipokuwa yeye mwenyewe. 13Amevaa joho lililochoviwa katika damu, na Jina lake ni “Neno la Mungu.” 14Majeshi ya mbinguni walikuwa wakimfuata, wakiwa wamepanda farasi weupe, hali wamevaa mavazi ya kitani safi, nyeupe na nzuri. 15Kinywani mwake hutoka upanga mkali ambao kwa huo atayaangusha mataifa. “Atayatawala kwa fimbo yake ya utawala ya chuma.” Hulikanyaga shinikizo la mvinyo wa ghadhabu ya Mungu Mwenyezi. 16Kwenye joho lake na paja lake pameandikwa jina hili:
Mfalme wa wafalme, na Bwana wa mabwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.