Ufunuo 18:5
Revelation 18:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
kwa kuwa dhambi zake zimelundikana hadi mbinguni, naye Mungu ameukumbuka uhalifu wake.
Revelation 18:5 in English
Revelation 18:5 · Berean Standard Bible
For her sins are piled up to heaven, and God has remembered her iniquities.
Context
3Kwa maana mataifa yote yamekunywa
mvinyo wa ghadhabu ya uasherati wake.
Nao wafalme wa dunia wamefanya uzinzi nao,
nao wafanyabiashara wa dunia
wametajirika kutokana na wingi wa utajiri wake.” 4Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni ikisema:
“Tokeni katikati yake, enyi watu wangu,
ili msije mkashiriki dhambi zake,
ili msije mkapatwa na pigo lake lolote; 5kwa kuwa dhambi zake zimelundikana hadi mbinguni,
naye Mungu ameukumbuka uhalifu wake. 6Mtendee kama yeye alivyotenda;
umlipe mara mbili kwa ajili ya yale aliyotenda.
Katika kikombe chake mchanganyie
mara mbili ya kile alichochanganya. 7Mpatie mateso na huzuni nyingi sawa na
utukufu na anasa alizojipatia.
Kwa kuwa moyoni mwake hujivuna, akisema,
‘Mimi ninatawala kama malkia;
mimi si mjane, wala sitaona huzuni kamwe.’
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.