Ufunuo 18:16
Revelation 18:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“ ‘Ole! Ole, ee mji mkubwa, uliyekuwa umevikwa mavazi ya kitani safi, ya rangi ya zambarau na nyekundu, ukimetameta kwa dhahabu, vito vya thamani na lulu!
Revelation 18:16 in English
Revelation 18:16 · Berean Standard Bible
saying: “Woe, woe to the great city, clothed in fine linen and purple and scarlet, adorned with gold and precious stones and pearls!
Context
14“Watasema, ‘Yale matunda ambayo roho yako iliyatamani yamekoma. Utajiri wako wote na fahari yako vimetoweka, wala haviwezi kupatikana tena kamwe!’ 15Wale wafanyabiashara waliotajirika kwa bidhaa hizo kutoka kwake watasimama mbali naye kwa hofu kubwa ya mateso yanayompata. Watalia na kuomboleza wakipiga kelele wakisema: 16“ ‘Ole! Ole, ee mji mkubwa,
uliyekuwa umevikwa mavazi ya kitani safi,
ya rangi ya zambarau na nyekundu,
ukimetameta kwa dhahabu,
vito vya thamani na lulu! 17Katika muda wa saa moja utajiri wote mkubwa
kama huu umeangamia!’
“Kila nahodha, na wote wasafirio kwa meli, na wote wapatao kipato chao kutokana na bahari, watasimama mbali. 18Watakapouona moshi wa kuungua kwake watalia wakisema, ‘Je, kulipata kuwako mji mkubwa kama huu?’
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.