Zaburi 39:3
Psalms 39:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Moyo wangu ulipata moto ndani yangu, nilipotafakari, moto uliwaka, ndipo nikasema kwa ulimi wangu:
Psalms 39:3 in English
Psalms 39:3 · Berean Standard Bible
My heart grew hot within me; as I mused, the fire burned. Then I spoke with my tongue:
Context
1Nilisema, “Nitaziangalia njia zangu
na kuuzuia ulimi wangu usije ukatenda dhambi;
nitaweka lijamu kinywani mwangu
wakati wote waovu wanapokuwa karibu nami.” 2Lakini niliponyamaza kimya na kutulia,
hata pasipo kusema lolote jema,
uchungu wangu uliongezeka. 3Moyo wangu ulipata moto ndani yangu,
nilipotafakari, moto uliwaka,
ndipo nikasema kwa ulimi wangu: 4“Ee Bwana, nijulishe mwisho wa maisha yangu
na hesabu ya siku zangu;
nijalie kujua jinsi maisha yangu
yanavyopita upesi. 5Umefanya maisha yangu mafupi kama pumzi;
muda wangu wa kuishi ni kama
hauna thamani kwako.
Maisha ya kila mwanadamu
ni kama pumzi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.