Mithali 9:11
Proverbs 9:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa maana kwa msaada wangu siku zako zitakuwa nyingi, na miaka itaongezwa katika maisha yako.
Proverbs 9:11 in English
Proverbs 9:11 · Berean Standard Bible
For through wisdom * your days will be multiplied, and years will be added to your life.
Context
9Mfundishe mtu mwenye hekima
naye atakuwa na hekima zaidi;
mfundishe mtu mwadilifu
naye atazidi kufundishika. 10“Kumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima,
na kumjua Aliye Mtakatifu ni ufahamu. 11Kwa maana kwa msaada wangu
siku zako zitakuwa nyingi,
na miaka itaongezwa katika maisha yako. 12Kama wewe una hekima, hekima yako itakupa tuzo;
kama wewe ni mtu wa mzaha,
wewe mwenyewe ndiwe utateseka.” 13Mwanamke aitwaye Mpumbavu ana kelele;
hana adabu na hana maarifa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.