Mithali 27:15
Proverbs 27:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mke mgomvi ni kama matone yasiyokoma ya siku ya mvua.
Proverbs 27:15 in English
Proverbs 27:15 · Berean Standard Bible
A constant dripping on a rainy day and a contentious woman are alike—
Context
13Chukua vazi la yule awekaye dhamana
kwa ajili ya mgeni;
lishikilie iwe dhamana kama anafanya hivyo
kwa ajili ya mwanamke mpotovu. 14Kama mtu akimbariki jirani yake kwa sauti kuu
asubuhi na mapema,
itahesabiwa kama ni laana. 15Mke mgomvi ni kama
matone yasiyokoma ya siku ya mvua. 16Kumzuia yeye ni kama kuuzuia upepo
au kukamata mafuta kwa kiganja cha mkono. 17Kama vile chuma kinoavyo chuma,
ndivyo mtu amnoavyo mwenzake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.