Mithali 14:2
Proverbs 14:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yeye ambaye njia zake ni nyofu humcha Bwana, bali yeye ambaye njia zake zimepotoka humdharau Mungu.
Proverbs 14:2 in English
Proverbs 14:2 · Berean Standard Bible
He who walks in uprightness fears the LORD, but the one who is devious in his ways despises Him.
Context
1Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake,
bali mpumbavu huibomoa nyumba yake
kwa mikono yake mwenyewe. 2Yeye ambaye njia zake ni nyofu humcha Bwana,
bali yeye ambaye njia zake zimepotoka humdharau Mungu. 3Mazungumzo ya mpumbavu huleta fimbo mgongoni mwake,
bali mwenye hekima hulindwa na maneno ya midomo yake. 4Pale ambapo hakuna mafahali, hori ni tupu,
bali kutokana na nguvu za fahali huja mavuno mengi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.