Wafilipi 1:21
Philippians 1:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa maana kwangu mimi, kuishi ni Kristo, na kufa ni faida.
Philippians 1:21 in English
Philippians 1:21 · Berean Standard Bible
For to me, to live is Christ, and to die is gain.
Context
19kwa maana ninajua kwamba kwa maombi yenu na kwa msaada unaotolewa na Roho wa Yesu Kristo, yale yaliyonipata mimi yatageuka kuwa wokovu wangu. 20Ninatarajia kwa shauku kubwa na kutumaini kwamba sitaaibika kwa njia yoyote, bali nitakuwa na ujasiri wa kutosha ili sasa kama wakati mwingine wowote, Kristo atukuzwe katika mwili wangu, ikiwa ni kwa kuishi au kwa kufa. 21Kwa maana kwangu mimi, kuishi ni Kristo, na kufa ni faida. 22Kama nitaendelea kuishi katika mwili, kwangu hili ni kwa ajili ya matunda ya kazi. Lakini sijui nichague lipi? Mimi sijui! 23Ninavutwa kati ya mambo mawili: Ninatamani kuondoka nikakae pamoja na Kristo, jambo hilo ni bora zaidi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.