Obadia 1:7
Obadiah 1:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wote ulioungana nao watakufukuza hadi mpakani, rafiki zako watakudanganya na kukushinda, wale wanaokula mkate wako watakutegea mtego, lakini hutaweza kuugundua.
Obadiah 1:7 in English
Obadiah 1:7 · Berean Standard Bible
All the men allied with you will drive you to the border; the men at peace with you will deceive and overpower you. Those who eat your bread * will set a trap for you without your awareness of it.
Context
5“Ikiwa wevi wangekuja kwako,
ikiwa wanyangʼanyi wangekujia usiku:
Lo! Tazama ni maafa kiasi gani yangekuwa yanakungojea:
je, si wangeiba tu kiasi ambacho wangehitaji?
Kama wachuma zabibu wangekuja kwako,
je, wasingebakiza zabibu chache? 6Lakini tazama jinsi Esau atakavyotekwa,
jinsi hazina zake zilizofichwa zitatekwa nyara! 7Wote ulioungana nao watakufukuza hadi mpakani,
rafiki zako watakudanganya na kukushinda,
wale wanaokula mkate wako watakutegea mtego,
lakini hutaweza kuugundua. 8“Katika siku hiyo,” asema Bwana,
“je, sitaangamiza watu wenye hekima wa Edomu,
watu wenye ufahamu katika milima ya Esau? 9Ee Temani, mashujaa wako watatiwa hofu,
kila mmoja katika milima ya Esau
ataangushwa chini kwa kuchinjwa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.