Obadia 1:20
Obadiah 1:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kundi la Waisraeli walioko uhamishoni Kanaani watarudi na kumiliki nchi mpaka Sarepta. Walioko uhamishoni Sefaradi kutoka Yerusalemu watamiliki miji ya Negebu.
Obadiah 1:20 in English
Obadiah 1:20 · Berean Standard Bible
And the exiles of this host of the Israelites will possess the land of the Canaanites as far as Zarephath; and the exiles from Jerusalem who are in Sepharad will possess the cities of the Negev.
Context
18Nyumba ya Yakobo itakuwa moto,
na nyumba ya Yosefu itakuwa mwali wa moto;
nayo nyumba ya Esau itakuwa bua kavu,
nao wataiwasha moto na kuiteketeza.
Hakutakuwa na watakaosalimika
kutoka nyumba ya Esau.”
Bwana amesema. 19Watu kutoka nchi ya Negebu
wataikalia milima ya Esau,
na watu kutoka miteremko ya vilima
watamiliki nchi ya Wafilisti.
Watayakalia mashamba ya Efraimu na Samaria,
naye Benyamini atamiliki Gileadi. 20Kundi la Waisraeli walioko uhamishoni Kanaani
watarudi na kumiliki nchi mpaka Sarepta.
Walioko uhamishoni Sefaradi kutoka Yerusalemu
watamiliki miji ya Negebu. 21Waokoaji watakwea juu ya Mlima Sayuni
kutawala milima ya Esau.
Nao ufalme utakuwa wa Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.