Native Bible

Numbers 7:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hivyo Mose akachukua yale magari ya kukokotwa pamoja na maksai, na kuwapa Walawi.

Numbers 7:6 in English

Numbers 7:6 · Berean Standard Bible

So Moses took the carts and oxen and gave them to the Levites.

Context

4Bwana akamwambia Mose, 5“Vikubali vitu hivi kutoka kwao, ili viweze kutumika katika kazi kwenye Hema la Kukutania. Wapatie Walawi kama kazi ya kila mtu itakavyohitaji.” 6Hivyo Mose akachukua yale magari ya kukokotwa pamoja na maksai, na kuwapa Walawi. 7Aliwapa Wagershoni magari mawili ya kukokotwa na maksai wanne, kama walivyohitaji kwa kazi yao, 8na pia aliwapa Wamerari magari manne ya kukokotwa na maksai wanane, kama kazi yao ilivyohitaji. Wote walikuwa chini ya maelekezo ya Ithamari mwana wa kuhani, Aroni.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.