Hesabu 7:29
Numbers 7:29 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Eliabu mwana wa Heloni.
Numbers 7:29 in English
Numbers 7:29 · Berean Standard Bible
and a peace offering of two oxen, five rams, five male goats, and five male lambs a year old. This was the offering of Eliab son of Helon.
Context
27fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 28mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; 29maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Eliabu mwana wa Heloni. 30Siku ya nne Elisuri mwana wa Shedeuri, kiongozi wa kabila la Reubeni, alileta sadaka yake. 31Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.