Hesabu 35:13
Numbers 35:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Miji hii sita mtakayoitoa itakuwa miji yenu ya makimbilio.
Numbers 35:13 in English
Numbers 35:13 · Berean Standard Bible
The cities you select will be your six cities of refuge.
Context
11chagueni baadhi ya miji iwe miji yenu ya makimbilio, ambayo mtu ambaye ameua mwenzake bila kukusudia aweza kukimbilia humo. 12Itakuwa mahali pa kukimbilia kutoka mlipiza kisasi, ili kwamba mtu aliyeshtakiwa kwa mauaji asife kabla ya kujitetea mbele ya mkutano. 13Miji hii sita mtakayoitoa itakuwa miji yenu ya makimbilio. 14Mtatoa miji mitatu ngʼambo hii ya Yordani na miji mingine mitatu upande wa Kanaani kama miji ya makimbilio. 15Miji hii sita itakuwa mahali pa makimbilio kwa ajili ya Waisraeli, wageni na watu wengine wanaoishi katikati yenu, ili kwamba mtu yeyote ambaye ameua mtu mwingine pasipo kukusudia aweze kukimbilia humo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.