Native Bible

Numbers 28:27 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mlete sadaka ya kuteketezwa ya mafahali wawili wachanga, kondoo dume mmoja, na pia wana-kondoo saba wenye umri wa mwaka mmoja, kama harufu nzuri ya kumpendeza Bwana.

Numbers 28:27 in English

Numbers 28:27 · Berean Standard Bible

Present a burnt offering of two young bulls, one ram, and seven male lambs a year old as a pleasing aroma to the LORD,

Context

25Siku ya saba mwe na kusanyiko takatifu na msifanye kazi zenu za kawaida. 26“ ‘Siku ya malimbuko, mnapomletea Bwana sadaka ya nafaka mpya wakati wa Sikukuu ya Majuma, mwe na kusanyiko takatifu na msifanye kazi zenu za kawaida. 27Mlete sadaka ya kuteketezwa ya mafahali wawili wachanga, kondoo dume mmoja, na pia wana-kondoo saba wenye umri wa mwaka mmoja, kama harufu nzuri ya kumpendeza Bwana. 28Pamoja na kila fahali itatolewa sadaka ya nafaka ya unga laini sehemu tatu za kumi za efa uliochanganywa na mafuta; pamoja na kondoo dume, andaa sehemu mbili za kumi za efa za unga laini; 29na sehemu ya kumi ya efa ya unga laini kwa kila mmoja wa wana-kondoo saba.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.