Native Bible

Numbers 28:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Pia mtoe beberu mmoja kama sadaka ya dhambi ambaye atafanya upatanisho kwa ajili yenu.

Numbers 28:22 in English

Numbers 28:22 · Berean Standard Bible

Include one male goat as a sin offering to make atonement for you.

Context

20Pamoja na kila fahali, andaa sadaka ya nafaka sehemu tatu za kumi za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta; pamoja na kondoo dume, andaa sehemu mbili za kumi za efa; 21pia pamoja na kila mmoja wa wale wana-kondoo saba, andaa sehemu ya kumi ya efa. 22Pia mtoe beberu mmoja kama sadaka ya dhambi ambaye atafanya upatanisho kwa ajili yenu. 23Andaa hizi licha ya zile sadaka za kawaida za kuteketezwa za kila asubuhi. 24Kwa njia hii andaa chakula cha sadaka ya kuteketezwa kila siku, kwa siku saba kama harufu nzuri impendezayo Bwana. Hii itaandaliwa licha ya ile sadaka ya kawaida ya kuteketezwa ya kila siku pamoja na sadaka yake ya kinywaji.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.