Hesabu 22:21
Numbers 22:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Balaamu akaamka asubuhi, akatandika punda wake akaenda pamoja na wakuu wa Moabu.
Numbers 22:21 in English
Numbers 22:21 · Berean Standard Bible
So in the morning Balaam got up, saddled his donkey, and went with the princes of Moab.
Context
19Mlale hapa usiku huu kama wale wengine walivyofanya, nami nitatafuta ni nini kingine Bwana atakachoniambia.” 20Usiku ule Bwana akamjia Balaamu na kumwambia, “Kwa kuwa watu hawa wamekuja kukuita wewe, nenda nao, lakini ufanye tu lile nitakalokuambia.” 21Balaamu akaamka asubuhi, akatandika punda wake akaenda pamoja na wakuu wa Moabu. 22Lakini Mungu alikasirika sana alipokwenda, naye malaika wa Bwana akasimama barabarani kumpinga. Balaamu alikuwa amepanda punda wake, na watumishi wake wawili walikuwa pamoja naye. 23Wakati punda alipomwona malaika wa Bwana akiwa amesimama barabarani akiwa na upanga uliofutwa mkononi mwake, punda akageukia upande kuelekea shambani. Balaamu akampiga ili amrudishe barabarani.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.