Native Bible

Numbers 13:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mwishoni mwa siku arobaini wakarudi kutoka kuipeleleza nchi.

Numbers 13:25 in English

Numbers 13:25 · Berean Standard Bible

After forty days the men returned from spying out the land,

Context

23Walipofika katika Bonde la Eshkoli, walivunja tawi lililokuwa na kishada kimoja cha zabibu. Wawili wao wakalichukua lile tawi kwenye mti, pamoja na komamanga na tini. 24Eneo lile likaitwa Bonde la Eshkoli kwa sababu ya kile kishada cha zabibu ambacho Waisraeli walikikata huko. 25Mwishoni mwa siku arobaini wakarudi kutoka kuipeleleza nchi. 26Wakarudi kwa Mose, Aroni na jumuiya yote ya Waisraeli huko Kadeshi kwenye Jangwa la Parani. Hapo ndipo walipotoa habari kwao na kwa kusanyiko lote na kuwaonyesha matunda ya hiyo nchi. 27Wakampa Mose taarifa hii: “Tuliingia katika nchi uliyotutuma, nayo inatiririka maziwa na asali! Hili hapa tunda lake.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.