Native Bible

Numbers 11:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Umande ulipoanguka kambini wakati wa usiku, pia mana ilianguka pamoja nao.

Numbers 11:9 in English

Numbers 11:9 · Berean Standard Bible

When the dew fell on the camp at night, the manna would fall with it.

Context

7Mana ilifanana kama mbegu za giligilani, nayo ilikuwa na rangi ya manjano iliyopauka. 8Hao watu walikwenda kukusanya, kisha waliisaga kwa mawe ya kusagia ya mkono au kuitwanga kwenye vinu. Waliipika vyunguni au kutengeneza maandazi. Ladha yake ilikuwa kama kitu kilichotengenezwa kwa mafuta ya zeituni. 9Umande ulipoanguka kambini wakati wa usiku, pia mana ilianguka pamoja nao. 10Mose akasikia watu wa kila jamaa wakilia, kila mmoja kwenye mlango wa hema lake. Bwana akakasirika mno, naye Mose akafadhaika. 11Akamuuliza Bwana, “Kwa nini umeleta taabu hii juu ya mtumishi wako? Nimekufanyia nini cha kukuchukiza hata ukaweka mzigo huu wa watu hawa wote juu yangu?

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.