Nehemia 6:5
Nehemiah 6:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Basi, mara ya tano, Sanbalati akamtuma msaidizi wake kwangu akiwa na ujumbe wa aina ile ile, naye alikuwa amechukua mkononi mwake barua isiyofungwa,
Nehemiah 6:5 in English
Nehemiah 6:5 · Berean Standard Bible
The fifth time, Sanballat sent me this same message by his young servant, who had in his hand an unsealed letter
Context
3Kwa hiyo niliwatuma wajumbe kwao na majibu haya: “Kazi ninayoifanya ni kubwa sana, siwezi kuja. Kwa nini niiache kazi isimame nije kwenu?” 4Mara nne walinitumia ujumbe wa namna iyo hiyo, na kila mara niliwapa jibu lile lile. 5Basi, mara ya tano, Sanbalati akamtuma msaidizi wake kwangu akiwa na ujumbe wa aina ile ile, naye alikuwa amechukua mkononi mwake barua isiyofungwa, 6iliyokuwa imeandikwa:
“Habari imeenezwa miongoni mwa mataifa, naye Geshemu anasema kwamba ni kweli, kuwa wewe na Wayahudi mnafanya hila ya kuasi, ndiyo sababu mnajenga ukuta. Zaidi ya hayo, kufuatana na taarifa hizi, karibuni utakuwa mfalme wao, 7na hata umewateua manabii wafanye tangazo hili kukuhusu wewe huko Yerusalemu: ‘Yuko mfalme katika Yuda!’ Sasa taarifa hii itarudishwa kwa mfalme. Basi njoo, tufanye shauri pamoja.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.