Native Bible

Nehemiah 3:31 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Baada yake Malkiya, mmoja wa masonara, alifanya ukarabati mpaka kwenye nyumba za watumishi wa Hekalu* na wafanyabiashara, mkabala na Lango la Ukaguzi, hadi kufikia chumba kilicho juu ya pembe.

Nehemiah 3:31 in English

Nehemiah 3:31 · Berean Standard Bible

Next to him, Malchijah, one of the goldsmiths, made repairs as far as the house of the temple servants and the merchants, opposite the Inspection Gate, and as far as the upper room above the corner.

Context

29Baada yao, Sadoki mwana wa Imeri alifanya ukarabati mkabala na nyumba yake. Baada yake, Shemaya mwana wa Shekania, mlinzi wa Lango la Mashariki, alifanya ukarabati. 30Baada yake, Hanania mwana wa Shelemia, na Hanuni mwana wa sita wa Salafu walikarabati sehemu nyingine. Baada yao, Meshulamu mwana wa Berekia alikarabati sehemu iliyokuwa mkabala na nyumba zake za kuishi. 31Baada yake Malkiya, mmoja wa masonara, alifanya ukarabati mpaka kwenye nyumba za watumishi wa Hekalu* na wafanyabiashara, mkabala na Lango la Ukaguzi, hadi kufikia chumba kilicho juu ya pembe. 32Masonara na wafanyabiashara walifanya ukarabati kutoka chumba kilichoko juu ya pembe hadi Lango la Kondoo.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.