Nehemia 3:28
Nehemiah 3:28 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Makuhani walifanya ukarabati juu ya Lango la Farasi, kila mmoja mbele ya nyumba yake.
Nehemiah 3:28 in English
Nehemiah 3:28 · Berean Standard Bible
Above the Horse Gate, each of the priests made repairs in front of his own house.
Context
26na watumishi wa Hekalu walioishi juu ya kilima cha Ofeli walikarabati hadi kufikia mkabala na Lango la Maji, kuelekea mashariki na ule mnara uliojitokeza. 27Baada yao, watu wa Tekoa walikarabati sehemu nyingine, kuanzia mnara mkubwa utokezao hadi ukuta wa Ofeli. 28Makuhani walifanya ukarabati juu ya Lango la Farasi, kila mmoja mbele ya nyumba yake. 29Baada yao, Sadoki mwana wa Imeri alifanya ukarabati mkabala na nyumba yake. Baada yake, Shemaya mwana wa Shekania, mlinzi wa Lango la Mashariki, alifanya ukarabati. 30Baada yake, Hanania mwana wa Shelemia, na Hanuni mwana wa sita wa Salafu walikarabati sehemu nyingine. Baada yao, Meshulamu mwana wa Berekia alikarabati sehemu iliyokuwa mkabala na nyumba zake za kuishi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.