Native Bible

Nehemiah 3:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Lango la Bondeni lilikarabatiwa na Hanuni na wakazi wa Zanoa. Walilijenga upya, na kuweka milango yake na makomeo na nondo mahali pake. Pia walikarabati ukuta wenye urefu wa mita 450 hadi Lango la Samadi.

Nehemiah 3:13 in English

Nehemiah 3:13 · Berean Standard Bible

The Valley Gate was repaired by Hanun and the residents of Zanoah. They rebuilt it, installed its doors, bolts, and bars, and repaired a thousand cubits * of the wall as far as the Dung Gate.

Context

11Malkiya mwana wa Harimu, na Hashubu mwana wa Pahath-Moabu walikarabati sehemu nyingine pamoja na Mnara wa Matanuru. 12Shalumu mwana wa Haloheshi, mtawala wa nusu ya wilaya ya Yerusalemu, alikarabati sehemu iliyofuatia akisaidiwa na binti zake. 13Lango la Bondeni lilikarabatiwa na Hanuni na wakazi wa Zanoa. Walilijenga upya, na kuweka milango yake na makomeo na nondo mahali pake. Pia walikarabati ukuta wenye urefu wa mita 450 hadi Lango la Samadi. 14Lango la Samadi lilikarabatiwa na Malkiya mwana wa Rekabu, mtawala wa wilaya ya Beth-Hakeremu. Alilijenga upya, na kuweka milango yake, na makomeo na nondo. 15Lango la Chemchemi lilikarabatiwa na Shalumu mwana wa Kolhoze, mtawala wa wilaya ya Mispa. Alilijenga upya, akaliezeka na kuweka milango yake, na makomeo na nondo mahali pake. Pia alikarabati ukuta wa Bwawa la Siloamu karibu na Bustani ya Mfalme, hadi kwenye ngazi zinazoshuka kutoka Mji wa Daudi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.